Psalms 6

Sala Kwa Ajili Ya Msaada Wakati Wa Taabu

Kwa mwimbishaji. Kwa ala za nyuzi za muziki. Mtindo wa sheminithi.
Sheminithi ni mtajo mmojawapo katika lugha ya uimbaji.
Zaburi ya Daudi.

1 bEe Bwana, usinikemee katika hasira yako,
wala usiniadhibu katika ghadhabu yako.
2 cUnirehemu Bwana,
kwa maana nimedhoofika;
Ee Bwana, uniponye,
kwa maana mifupa yangu
ina maumivu makali.
3 dNafsi yangu ina uchungu mwingi.
Mpaka lini, Ee Bwana, mpaka lini?

4 eGeuka Ee Bwana, unikomboe,
uniokoe kwa sababu ya fadhili zako.
5 fHakuna mtu anayekukumbuka
akiwa amekufa.
Ni nani awezaye kukusifu
akiwa kuzimu?

6 gNimechakaa kwa kulia kwa huzuni;
usiku kucha nafurikisha
kitanda changu kwa machozi;
nimelowesha viti vyangu vya fahari
kwa machozi.
7 hMacho yangu yamedhoofika kwa kuhuzunika,
yamedhoofika kwa sababu ya adui zangu wote.

8 iKaeni mbali nami, ninyi nyote mtendao mabaya,
kwa maana Bwana amesikia kulia kwangu.
9 j Bwana amesikia kilio changu kwa huruma,
Bwana amekubali sala yangu.
10 kAdui zangu wote wataaibika na kufadhaika,
watarudi nyuma kwa aibu ya ghafula.
Copyright information for SwhNEN